Fredrick Sumaye akihutubia |
Fredrick Sumaye akisalimia na wanamichezo wenye ulemavu |
Mkurugenzi wa BQ Constuction akiwahutubia wanamichezo |
Mwenyekiti wa kamati ya Paralimpiki Tanzania akiwasalimu wanamichezo |
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye leo alikuwa mgeni rasmi kwenye kufunga mashindano ya tenisi kwa watoto wenye umri wa miaka nane hadi 18 na watu wenye ulemavu yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya Gymkhana na kudhamini na BQ Constructiion.
Mashindano haya yalishirikisha watoto toka kwenye mikoa ya Arusha, Morogoro na Dar es Salaam yamefana na walionyesha vipaji vya kucheza tenisi.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Chama cha tenisi Inger Njau alisema kuwa wachezaji watakaoshinda wataiwakilisha nchi kwenye mashin dano ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika nchini Kenya mwakani.
Akizungumza na wanamichezo kabla ya kutoa zawadi waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye aliipongeza kampuni ya BQ kwa kudhamini mashindano haya hasa kwa watoto na watu wenye ulemavu kwani kwa Mungu atapata thawabu.
"Mungu atakupa thawabu kwa kuwakumbuka watoto na watu wenye ulemavu kwani kutokana na jinsi nilivyochoka ingekuwa mashindano mengine nisingekuja.
Sumaye alisema alishuka uwanja wa ndege majira ya saa tisa akitokea China.
No comments:
Post a Comment