Michuano ya Kombe la Uhai
inayoshirikisha timu B za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia
kuanza Desemba 7 mwaka huu na kumalizika Desemba 22 mwaka huu.
Mashindano haya ambayo yamedhaniwa na kampuni ya Azam kupitia bidhaa yake ya maji ya Uhai yatashirikisha wachezaji ambao usajili wao ulifanyika na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni. Hakutakuwa
na usajili mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi
Kuu labda kama timu ilisajili wachezaji 22 tu ndizo zitakazo ruhusiwa kuongeza.
Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hii
No comments:
Post a Comment