KIKOSI CHA NMB |
TASWA FC |
Mbozi Katala wa TASWA FC na Pastory wa NMB wakipambana kwenye mchezo wa awali, hata hivyo walitoka sare ya 1-1 |
Azam Group |
Gymkhana FC |
Bonanza hili limedhaminiwa na kampuni ya Vennedrick (T) Limited kupitia Mkurugenzi wake Fredrick Mwakalebela na kudhaminiwa na NMB banki.
Bonanza hili linaendeshwa kwa mtindo wa ligi na timu mbili toka kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali na
Timu za Barrick, NMB, DSTV na Radio Times zipo kundi A na TASWA FC, Jubilee, Azam Group na wenyeji Gymkhana wapo kundi B
Mchezo wa awali Gymkana waliifunga Azam bao 1-0 na katika mchezo wa pili Gymkhana wakaifunga Barrick mabao 3-1
NMB walitoshana nguvu na TASWA FC baada ya sare ya 1-1 na NMB wametoka suluhu na Times FM ya 0-0.
Michezo mingine Times wameifunga Jubilee bao 1-0, Azam walifungwa n Dstv bao 2-1, Jubilee wakifunga TASWA bao 1-0,
Kwenye michezo ya nusu fainali timu zilionyeshana umamba wa kupigana badala ya soka la uwanjani kwani TASWA walitolewa na waandaaji baada kutokea fujo wakati wa mchezo wao na Gymkhana, Gymkhana walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0
Mchezo mwingine wa nusu fainali nao haukumalizika kwa NMB waliondoa timu uwanjani wakati Dstv wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0
Fainali nayo pia hakumalizika kwani Dstv walifanya fujo na mchezaji wao alipoonyeshwa kadi nyekundu waligoma kuendelea na kutoa timu uwanjani.
Waandaji wakatangaza Gymkhana kuwa mabingwa na timu yenye nidhamu wakiwa ni times Fm na kukabidhiwa kikombe kila mmoja
No comments:
Post a Comment