Madrid
WAKATI Lionel Messi akiifungia mara mbili Barcelona na
kuipa ushindi wa 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Mfalme "Copa del Rey"
dhidi ya Cordoba usiku wa kuamkia jana, Celta Vigo iliinyuka Real Madrid 2-1
katika kinyang'anyiro hicho.
Mario Bermejo na Cristian Bustos ndiyo
walioiwezesha Celta kuongoza kwa mabao 2-0 kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga
bao la usiku na kurejesha matumaini kwa Real kuingia katika mzunguko wa pili.
No comments:
Post a Comment