Hatimaye uongozi wote wa juu wa TOC umerudi tena madarakani baada ya uchaguzi uliofanyika kwenye hotel ya Dodoma mjini Dodona. Habari zaidi tutaendelea kuwafahamisha
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF Fredrick Mwakalebela ameangushwa na Filbert Bayi ambaye alikuwa anatetea nafasi yake.
Nafasi ya Urais imekwenda kwa Gulam Rashid ambaye alipata kura 44 huku mpinzania wake Khamis Abdallah akiambulia kura 12
Makamu wa Rais ni Hassan Jaruf kura 31, Henry Tandau kura 19 na Abdulhakim Cosmas aliambulia kura 1
Katibu Mkuu, Filbert Bayi alipata kura 45, Fredrick Mwakalebela kura 10 na Juma Ikangaa aambulia kura moja
Nafasi ya Katibu msaidizi imekwenda kwa Jamal Nassor aliyepata kura 45 na David Mwakiposa aliambulia kura 10
Charles Nyange aliukwaa mwka hazina baada ya kupata kura 50 na mweka hazina msaidizi ni Juma Hamis
Wajumbe kwa upande wa Tanzania Bara ni Noorelain Sharif kura 47, Irene Mwakisanga kura 44, Lina Kessy kura 43, Muharam Mchome kura 37 na Suleiman Nyambui kura 37
Wajumbe kwa upande wa Zanzibar ni Nasra Juma kura 48, Sukleiman Jabir kura 43, Suleiman Ame kura 38, Mussa Abdul kura 37, Saadun Ahmed kura 35
Olypians bara ni Samwel Mwera na Fabian Joseph
Athletics commission Makame Ally kura 27
No comments:
Post a Comment