KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernie
Brandts, yupo hoi baada ya jana kushindwa kutokea katika mazoezi huku klabu
hiyo ikibebeshwa mzigo wa kuwatema wachezaji ambao hawatakuwemo katika mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mazoezi hayo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama Dar es Salaam, imeelezwa
Brandts anaumwa malaria na kusababisha kushindwa kuendelea na programu ya
kuwanoa wachezaji wa timu hiyo.
Daktari wa timu hiyo, Juma
Sufiani alithibitisha, Brandts kushindwa kuendelea na majukumu yake kutokana na
kuumwa ugonjwa huo.
Yanga
ambayo inajiandaa kwenda kuweka kambi ya wiki moja Uturiki katika mazoezi ya
jana yalisimamiwa na Kocha Msaidizi, Fred Minziro, ambayo yalifanyika kwa saa
tatu.
Wakati huo huo, Uongozi wa
klabu hiyo, umempa rungu Brandts kuhakikisha anawakata wachezaji ambao
hawakuwamo katika kikosi chake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam
jana, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema wameamua kurejesha
suala hilo kwa Brandts kutokana na awali alipendekeza baadhi ya wachezaji
wapelekwe mkopo ama waache katika usajili mdogo wa ligi hiyo.
Sanga alisema kwa kuwa
Brandts alipendekeza majina ya wachezaji wa kuachwa kwa Kamati ya mashindano ya
klabu hiyo, wamemtaka achague kutokana na wengine, bado wana mikataba na klabu
hiyo.
Alisema wachezaji wengine
hawatakiwi kuachwa kutokana na wana mikataba, kwani anatakiwa aangalie upya.
Sanga alisema usajili huo unatarajia kukamilika wiki
hii.
No comments:
Post a Comment