TIMU ya Moro United inayoshiriki ligi daraja la kwanza juzi zilitoshana nguvu na Ndanda FC ya Mtwara kwa kufungana bao 1-1 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Karume jijini, Dar es Salaam.
Ndanda ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya kwanza kupitia kwa Elias Ndokezi lakini Moro walisawazisha bao hilo dakika ya 30 kupitia kwa Gideon Benson.
Timu zote zilikwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko lakini hakuna timu iliyoweza kuongeza bao.
Kocha wa Ndanda Amri Ibrahim alisema wachezaji wake hasa safu ya viungo na washambuliaji wamesababisha kupoteza mchezo huo kwani walikosa nafasi nyingi za wazi za kufunga.
"Washambuliaji na viungo wamesababisha tupoteze mchezo ila tutajipanga turekebishe makosa", alisema Amri.
Naye kocha wa Moro United, Mwinyi Kassembo alisema wanashukuru kwa matokeo hayo kwani yanatia matumaini kutokana na kuwa alipokea timu ikiwa haina pointi baada ya kucheza michezo mitatu.
"Nashukuru leo ni mchezo wa pili tunatoka sare baada ya kupokea timu ikiwa haina pointi", alisema Kassembo.
Awali Moro ilikuwa inafundishwa na Yusuph Macho na kutokana na matokeo mabovu uongozi uliamua kumfukuza.
Uwanja wa Mabatini, Pwani timu ya Polisi ya Dar es Salaam ilipokea kipigo cha bao 1-0 toka kwa Tesema ya Temeke.
No comments:
Post a Comment