ANDRE Villas-Boas,
amesema yeye ndiyo anastahili lawama baada ya timu yake ya Tottenham Hotspurs, kupoteza
nafasi ya kuwafunga mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City, na
kujikuta wakilala kwa mabao 2-1.
Tottenham walionekana
kuwa na nafasi ya kushinda pambano hilo baada ya kuanza kufunga kupitia kwa Steven
Caulker katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza.
Lakini AVB amekiri
kwamba kocha wa Man City, Roberto Mancini alifanya mabadiliko sahihi katika
kipindi cha pili cha mchezo huo na kuamua kutumia mabeki watatu.
AVB alishindwa kujibu
mapigo na kujikuta akilala kwenye pambano hilo baada ya Sergio Aguero
kuirudisha Man City mchezoni na supa sub Edin Dzeko akafunga bao la ushindi.
Kocha huyo alisema
kwamba wakati matokeo yakiwa 1-1 aliamua kupaki basi ilikupata sare lakini
kitendo hicho kiliwapa nafasi Man City kuwashambulia sana kitu kilichoamsha
mashabiki, na kufanya mechi kuwa ngumu kwao kutokana na mashambulizi mfululizo
ya Man City mpaka pale Dzeko alipofunga bao la ushindi
No comments:
Post a Comment