Timu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa pamoja na viongozi wao |
Timu ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania |
Watoto wakielekezwa jinsi ya kuanza mchezo kuashiria ufunguzi kwenye viwanja vya Leader Club Kinondoni |
Waamuzi na timu wakisubiri mgeni rasmi |
Watoto wakielekezwa jinsi ya kukabidhi zawadi na mkurugenzi wa UN nchini Tanzania Alberic Kacou |
Timu ya soka ya wafanyakazi wa UN wakiwa na kaombe lao. |
Timu ya soka ya Mambo ya Nje wakiwa na kombe walilotwaa |
Timu ya Soka ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imeifunga Umoja wa Mataifa kwa penalti 4-1 mchezo ulichezwa uwanja wa Leaders Club Kinondoni.
Mchezo huo ambao ulikuwa maalum kuadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ambayo itafikia kilele chake Octoba 24 mwaka huu imeanza kwa shamrashamra mbalimbali ikiwa kukutana na wafanyakazi wa serikali ya Tanzania na kubadilishana mawazo na uzoefu katika kazi.
Mchezo ulikuwa wa ushindani sana kwani mpaka mapumziko mambo ya nje walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko na UN wakafanikiwa kusawazisha bao hilo. Mpaka mwamuzi anamaliza mchezo matoeo 1-1 ndipo iliamuliwa zipigwe penalti na Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kupata penalti 4-1.
Vile vile kulikuwepo michezo wa kuvuta kamba ambapo UN walishinda dhidi ya mambo ya nje na mbio za magunia ambazo zilikuwa ni za kujifurahisha na michezo mabalimbali ya watoto.
Wafanyakazi wa UN wakivuta kamba kwenye uwanja wa Leader Club |
Watoto wa kike na wa kiume wa wafanyakazi wa UN wakivuta kamba |
Watoto wakichuana kwenye mbio cha magunia |
Wafanyakazi wa UN wakichuana kwenye mbio za magunia |
Watoto wakicheza |
No comments:
Post a Comment