Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 5, 2012

SERENGETI BOYS YAFUZU RAUNDI YA TATU



Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" imefuzu kucheza raundi ya tatu ya mashindano ya vijana baada ya Misri kujitoa.

Serengeti boys ambayo ilikuwa icheze nyumbani Octoba 14 na ingerudiana baada ya wiki mbili na Misri imefuzu kucheza hatua ya tatu ambayo ni ya mwisho. 

Katika raundi ya kwanza Serengeti Boys inayofundishwa na Jakob Michelsen kutoka Denmark ilikuwa icheze na Kenya mwezi uliopita, lakini nchi hiyo ilijitoa katika michuano hiyo ambayo fainali zake zitachezwa Machi mwakani nchini Morocco.

Serengeti Boys sasa itacheza raundi ya tatu kwa kumkabili mshindi wa mechi kati ya Zimbabwe na Congo Brazzaville. Mechi ya kwanza itachezwa Novemba 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati ya marudiano itafanyika ugenini wiki mbili baadaye.

Zimbabwe na Congo Brazzaville zitacheza  kati ya Oktoba 12-14 mwaka huu, Zimbabwe ikiwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, wakati ya marudiano itafanyika kati ya Oktoba 26-28 mwaka huu.

Kikosi cha Serengeti boys ambayo kiufundi inaonekana ipo vizuri inatakiwa iendelee kujifua zaidi ili iweze kuwapa raha watanzania kwa kushinda raundi ya tatu na kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye fainali za vijana mwakani nchini Morocco 

No comments:

Post a Comment