Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 10, 2012

MASHINDANO YA RIADHA YAFUNGWA

  
Wanariadha wa kike mita 400

Mbia mita 400 wanaume wakichuana fainali

Wanaume riadha wakiruka vihunzi

Add caption

Mrusha tufe wanawake akijiandaa kurusha tufe

 MWENYEKITI wa baraza la michezo Jamal Malinzi juzi alifunga mashindano ya riadha yaliyokuwa yanafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia Septemba 7 mwaka huu.

Akizungumza na wanamichezo Malinzi alisema anawapongeza wale wote walioshiriki kwani kwa kushiriki ni moja ya sifa na kupata medali ni sifa nyingine. Pia alivitaka vyama vya wilaya na mikoa kuandaa mashindano ili kupata washiriki wazuri na watakaoleta changamoto.
"Vyama vya wilaya na mikoa andaeni mashindano ili mpate washiriki wazuri watakao kuja kushindana na naamini huko chini ndio kuna vipaji", alisema Malinzi.

Pia aliagiza Chama cha riadha R.T kuchunguza kwanini Tanzania  haikuweza kupata medali kwenye mashindano ya Olympic iliyomalizika hivi karibuni jijini London na kauli ya R.T juu ya mashindano ya riadha yanayoendelea jijini Arusha wakati R.T nao wanaendesha mashindano ya kitaifa.

"Nangoja kauli ya R.T juu ya mashindano ya riadha yanayoendelea jijini Arusha wakati nyie chama cha Taifa mnaendesha mashindano ya Riadha ya Taifa na R.T ndio mnapaswa kutoa vibali vya riadha nchi hii", alihoji Malinzi

Malinzi bila kutaja chama wala mtu alivishukia vyama na wajumbe ambao ndio wapiga kura kwa kuchagua viongozi ambao ni wezi, matapeli na mafisadi kwa sababu ya kuhongwa pesa kidogo, kauli ambayo ilifanya ashangiliwa na wanamichezo kiasi kwamba walitaka aendelee kuongea maana maneno yake yalikuwa yanagusa uhalisia.

Timu ya Mjini Magharibi toka Zanzibar iliibuka mshindi wa jumla kwa kupata medali 30,dhahabu 17, fedha 10 na shaba 3, Arusha walishika nafasi ya pili kwa kupata medali 26, dhahabu 4, fedha 12 na shaba 10 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Kilimanajaro ambao walipata medali 8, dhahabu 3 fedha 2 na shaba 2 huku mkoa wa Dar es salaam, ambao ni mwenyeji ukiambulia nafasi ya tano kwa kupata medali 6.

Kwa upande wa Wanawake Mjini Magharibi walikuwa wa kwanza kwa kupata medali za dhahabu 7, fedha 3 na shaba 2, Arusha ilishika nafasi ya pili kwa kupata dhahabu 4, fedha 8 na shaba 4na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Tabora ambayo ilipata dhahabu 1 fedha 3 na shaba 4.

Upande wa wanaume Arusha ilikuwa kidedea kwa kuondoka na medali za dhahabu 4, fedha 8 na shaba 5, nafasi ya pili ilikwenda kwa Mjini Magharibi ambao walondoka na medali za dhahabu 7, fedha 3 na shaba 2.

Wakati wa kusoma washindi almanusura iingie dosari baada ya aliyekuwa anasoma kutangaza mshindi wa jumla ni Arusha sababu iliyowafanya Zanzibar kupiga kelele na kusema hawataki kwani weo ndio washindi kutokana na medali walizokuwa nazo. Marekebisho yakafanyika na kugundua ni kweli Mjini Magharibu ndio washindi na Arusha wakiwa mshindi wa pili.

Zawadi kwa washindi zilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza la michezo Tanzania, Ndugu Jamal Malinzi baada ya kuzungumza na wanamichezo.

Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa zawadi kwa washindi Rais wa R.T Anhony Mtaka alisema jumla ya wanamichezo 461 wameshiriki na viongozi 84 toka Tanzania Bara na Zanzibar kwenye mashindano haya ambayo ni ya 51.Mikoa ambayo haikupata medali ni Kigoma, Ruvuma, Morogoro na Mbeya.

Nao wanamichezo walisikitishwa na kukosa vifaa kwani baadhi walikuwa wanakimbia bila viatu pia wanasikitishwa na kitendo cha ubinafisi wa wanariadha wanaopelekwa Olympic kutoshiriki kwani inaonyesha kuwa hawana uwezo na wanajiuliza hivyo viwango vya kushiriki wanavipatia wapi.

"Tunataka mashindano ya kuchagua timu ya kushiriki mashindano ya kimataifa kwani tunaamini sisi tuna uwezo zaidi ya hao wanawakilisha nchi na ndio maana leo hapa hakuna hata mmoja", alisema Najma George toka Zanzibar.

No comments:

Post a Comment