Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 1, 2012

KOZI YA WAAMUZI YAFUNGULIWA

Mkufunzi Leslie Liunda akifundisha sheria ambazo zimefanyiwa marekebisho na IFAB

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF akifungua semina ya waamuzi jana


Waamuzi wakimsikiliza Mkufunzi Leslie Liunda ( hayupo) wakati akifundisha marekebisho ya sheria za soka  yaliyofanywa na FIFA kupitia IFAB

MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni amewaasa waamuzi kutumia filimbi yao vizuri ili kutenda haki wanapo kuwa uwanjani.

Kayuni aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa  semina ya waamuzi wa daraja la kwanza kituo Dar es salaam iliyofanyika juzi, Uwanja wa Taifa, kwa ajili ya Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu wa 2012/13.

Alisema waamuzi ni kiungo muhimu  katika kuendeleza mpira nchini, endapo watakuwa mahakimu wazuri wakiwa uwanjani.

Aliwataka waamuzi hao  kuchezesha kwa kufuata sheria 17 za soka, ili waweze kusaidia soka la Tanzania kusonga mbele.

Kayuni aliwatahadharisha kuwa wanapochezesha vibaya wanajiharibia wao wenyewe, kwani mchezo wa soka una mashabiki wengine na unaonyeshwa karibu kila sehemu kutokana na teknolojia kukua.

"Endapo mtarubuniwa na viongozi wa vyama vya soka FA wanapokwenda kuchezesha mtoe taarifa kwa maandishi katika  ofisi yangu itawashughulikie kulikoni waamuzi kuendelea kuumia au kuwa mbuzi wa kafara," alisema Kayuni.

Hata hivyo, alisema amekuwa akisikia malalamiko kwa pembeni, lakini hajafikishiwa kwake.

Alisema amepata taarifa kuwa wanapokwenda mikoani kuchezesha viongozi wa FA wanawashinikiza timu zao zishinde na mnapoacha kutekeleza matakwa yao wanawanyima posho zao.

Jumla ya waamuzi wapatao 190 kutoka mikoa yote wameudhuria semina na kufanya mtihani ya utimamu  wa mwili. Semina hii inaratajiwa kufungwa kesho jioni.

No comments:

Post a Comment