NAIBU WAZIRI MAKONDA AWASILI MOROCCO KUIPA MORALI TAIFA STARS
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda amewasili nchini Morocco kwa lengo la kuipa nguvu na kuongeza morali kwa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanaume Taifa Stars, inayoshiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika AFCON 2025, nchini Morocco.
Mhe. Makonda ameenda nchini Morocco kuiwakilisha Serikali katika kuwaunga mkono wachezaji na benchi la ufundi la Taifa Stars, ili kuhakikisha timu inapata hamasa na kujiamini kwenye michezo itakayoshindana.
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Makonda alipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda, akiambatana na Bw. Abel Philip, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara pamoja na Profesa Madundo Mtambo, Mjumbe wa kamati ya kitaifa ya maandalizi ya AFCON 2027.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza tarehe 23 Desemba, 2025, katika mji wa Fes, Morocco, dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria.
Post a Comment