Pages

Tuesday, August 29, 2023

JKT QUEENS KUIVAA CBE FAINALI CECAFA

JKT Queens kesho itashuka dimbani kuikabili CBE ya Ethiopia katika mchezo wa fainali michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa ajili ya kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 9:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Njeru, nchini Uganda.
JKT ilitinga hatua hiyo baada ya kuiondosha Buja Queens ya Burundi mabao 3-1 huku CBE ya Ethiopia ikiiondosha Vihiga Queens ya Kenya kwa mabao 2-1.


No comments:

Post a Comment