Pages

Sunday, August 27, 2023

JKT QUEENS, CBE QUEENS KUCHEZA FAINALI CECAFA JUMATANO

 

CBE QUEENS

JKT QUEENS


Na Rahel Pallangyo

JKT Queens imetinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake kwa ukanda wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa kuifunga Buja Queens ya Burundi kwa mabao 3-1 Uwanja wa FTC Njeru, Kampala leo

Kwa ushindi huo JKT Queens itacheza fainali na  CBE ya Ethiopia ambayo iliifunga Vihiga Queens ya Kenya kwa mabao 2-1, Jumatano ijayo Agosti 30, 2023.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ulioanza saa 6:00 mchana JKT Queens walikwenda mapumziko wa kiwa nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Teopistar Situma dakika ya 11.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku JKT wakionekana kubadilika kwani waliliandama lango la Buja Queens na dakika ya 61 Donisia Minja alifungua kitabu cha mabao akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa wa Buja uliotokana na shuti la Stumai Abdallah.


Katika kuonesha kuwa JKT Queens wanahitaji kufuzu fainali dakika ya 77, kiungo mfupi  mwenye makeke uwanjani Stumai Abdallah alifunga bao la pili akimalizia mpira wa krosi iliyopigwa na Amina Bilal na kuibua shangwe kwa mashabiki na benchi la ufundi.

Wanasema haiwezi kuisha bila kumalizika kabisa kwani JKT Queens ambao walikuwa na uchu wa mabao zaidi, mshambuliaji kinda Winifrida Gerald alifunga bao la tatu kwenye dakika za nyongeza akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Anastazia Katunzi baada ya Stumai kufanyiwa madhambi.

JKT Queens katika makundu waliifunga AS Kigali ya Rwanda mabao 2-1 kabla ya kuibamiza New Generation ya Zanzibar bao 1-0 kisha kuikandamiza Vihiga Queens ya Kenya bao 1-0.

Mwisho

No comments:

Post a Comment