YANGA
imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC ugenini katika mchezo wa Ligi
Kuu Soka Tanzania Bara uliochezwa leo kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Aidha,
mchezaji wa Azam FC Abubakari Salum ‘Sure boy’ alitolewa kwa kadi nyekundu
baada ya kumsukuma Hassan Kessy mbele ya mwamuzi wa kati Israel Nkongo.
Azam ndio
ilikuwa ya kwanza kupata bao la uongozi dakika ya tatu baada ya kuanza kwa
mchezo huo likifungwa na Shaban Chilunda huku Obrey Chirwa akisawazisha dakika
ya 30 na la ushindi likifungwa na Gadiel Michael.
Ushindi huo
umeendelea kuibakiza Yanga katika nafasi
ya tatu kwenye msimamo ikifikisha jumla ya pointi 28, nyuma ya Azam yenye
pointi 30 na Simba 32.
Azam FC
ilianza mpira kwa kasi na kufanikiwa kupata bao hilo la uongozi baada ya
Chilunda kutengenezewa pasi na Bruce Kangawa.
Baada ya
Azam kuongoza bao hilo walianza kupunguza kasi na kuwapa nafasi wapinzani wao
kusawazisha kupitia kwa Chirwa aliyepata pasi ya Ibrahim Ajibu ambapo
alimzunguka kipa Razaki Abalora na kufunga.
Azam baada
ya kusawazishiwa walirudi tena kwenye kasi na kufanya mashambulizi mengi lakini
hayakuzaa matunda, na kutoa nafasi zaidi kwa Yanga kujiamini ambapo Gadiel
alipiga shuti kali nje ya 18 na kuifungia Yanga bao la pili.
Hadi kipindi
cha kwanza kinamalizika Azam ilikuwa ikiongoza kwa mashambulizi lakini Yanga
ilikuwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha
pili Azam iliendeleza kasi ya mashabulizi bila mafanikio kwani tayari Yanga iliweka ukuta na kupata wakati
mgumu wa kufunga. Hadi mpira unakwisha matokeo hayo
Kocha wa
Azam alijaribu kufanya mabadiliko kadhaa lakini hayakuzaa matunda. Dakika 36
alimtoa Bernard Arthur na kumuingiza Salmin Hoza, pia, kipindi cha pili dakika
55 na 65 alimtoa Stephen Kingue na Shaban Chilunda na kuingia Mbaraka Yusufu na
Paul Peter.
Kwa upande
wa Yanga dakika ya 66 iliwatoa Emmanuel Martin na kuingia Geofrey Mwashiuya,
pia, dakika 68 alimtoa Ibrahim Ajibu na kuingia Juma Mahadhi.
Azam
FC.Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Agrey Morris, Yakubu Mohamed,
Stephan Kingue, Salum Abubakari, Joseph Mahundi, Bernard Arthur, Shaban
Chilunda na Enock Atta.
Kikosi cha
Yanga. Youthe Rostand, Kelvin Yondani, Gadiel Michael, Hassan Kessy, Raphael
Daud, Andrew Vicent, Said Juma, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim
Ajibu na Emmanuel Martin.
Mechi
nyingine zilizochezwa ni Mwadui dhidi ya Njombe waliopata sare ya mabao 2-2 na
Mbeya City dhidi ya Mtibwa sare ya bila kufungana 0-0. Na Kagera Sugar na Lipuli
pia zikitoka sare ya 0-0.
No comments:
Post a Comment