MSIMAMIZI wa
kituo cha Mtwara, Dustan Mkundi ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Utendaji ya
TFF amefungiwa maisha kujihusisha na soka na kamati ya maadili ya Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) leo.
Mkundi na
wenzake wanne walipelekwa na sekretarieti TFF
kwenye kamati ya Maadili viongozi kwa kosa la kughushi na udanganyifu wa mapato
ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba na Ndanda FC uliochezwa
kwenye Uwanja wa Nangwanda Mtwara Desemba 30, 2017.
Akizungumza leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Wakili Hamidu Mbwezeleni
ambaye alisema kamati yake imewakuta na hatia Mkundi na
kumfungia maisha kujihusisha na soka na Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara
Kizito Mbano akafungiwa miaka mitano
Pia Mbwezeleni alisema Muhasibu msaidizi wa
Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa Klabu ya Ndanda FC ya Mtwara
Selemani Kachele hawakuwa na hatia.
“Sekretarieti iliondoa jina la Kahumbu kwenye
mashtaka badala yake aligeuka kuwa shahidi katika kesi hiyo lakini Mkundi
tulimkuta na hatia kwa sababu hesabu za mapato zilizopelekwa bodi ya ligi na
TFF zimetofautiana,”
“Bodi ya ligi alipekeleka mapato ya sh milioni
37 lakini TFF aliwasilisha sh milioni 34 na timu za Ndanda na Simba zilipata
mgao kutoka kwenye sh. milioni 37 hivyo udandanyifu ulifanyika katika mgao
uliohusu TFF, BMT na TRA,” aliongeza Mbwezeleni.
Mbwezeleni alisema Mkundi aliwapelekea fomu
nyingine Kahumbu na Kachele wamsainie kwa madai fomu za awali zilipotea na
wawili hao waliisadia kamati kupata undani wa mapato lakini Mbano hakuwa tayari
kukutana na kamati japo aliitwa mara tatu.
Aidha kamati hiyo imeitaka TFF kuhakikisha
wanalifikisha suala hilo kwenye vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.
Kamati ya maadili iko chini ya Mwenyekiti
Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti Wakili Steven Zangira, wajumbe ni
Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa.
No comments:
Post a Comment