Pages

Sunday, October 15, 2017

OKWI MCHEZAJI BORA SIMBA, AGOSTI -SEPTEMBA

Image result for OKWI EMMANUEL

MSHAMBULIAJI wa Simba Emmanuel Okwi ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo kwa Agosti-Septemba.
Katika taarifa ambayo imewekwa kwenye Simba App inasema Pamoja na tuzo hiyo Okwi amezawadiwa kitita cha sh 500,000 baada ya kuwapiku nyota wenzake kwenye idadi ya kura zinazopigwa na mashabiki wa timu hiyo kupitia
Okwi anakuwa mchezaji wa kwanza kutwaa tuzo hiyo tangu ibadilishwe jina na kuitwa ‘Simba App Player of the Month’.
Okwi anaongoza katika orodha ya wafungaji bora wa ligi kuu ya Vodacom akiwa amefunga mabao saba katika mechi tano ambazo amecheza japo Simba imecheza mechi sita.

No comments:

Post a Comment