Pages

Sunday, October 8, 2017

HUYU NDIE JULIANA SHONZA NAIBU WAZIRI WA MICHEZO



Juliana Shonza
RAIS  Dk John Magufuli amefanya mabadiliko katika Baraza lake la Mawaziri, ambapo amemteua Juliana Shonza kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilisema katika mabadiliko hayo, Waziri anaendela kuwa Dk. Harrison Mwakyembe.
Shonza ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) na wateule wengine wote wanatarajiwa kuapishwa Ikulu, Dar es Salaam kesho.
Katika mabadiliko hayo Rais Magufuli, amewahamisha baadhi ya mawaziri kwenda wizara nyingine, kuwapandisha baadhi ya manaibu waziri kuwa mawaziri kamili, kuwaingiza wapya na kuwaacha baadhi yao nje ya Baraza hilo, akiwemo aliyekua Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.

Mabadiliko hayo, pia yameongeza wizara kutoka 19 za awali kwa kuzigawanya baadhi ya wizara hizo na kufanya jumla ya wizara zote kuwa 21. 

No comments:

Post a Comment