Pages

Saturday, September 23, 2017

YANGA POINTI SAWA NA SIMBA





KIUNGO mshambuliaji wa Yanga Ibrahim Ajib amekuwa shujaa wa mchezo baada ya kuifungia timu yake bao pekee dhidi ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam/
Ajib ambaye leo alitajwa na kocha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga kwenye kikosini kitakachoingia kambini Oktoba Mosi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Malawi amemdhihiriwa Mayanga kuwa hakukosea baada ya kufunga bao hilo pekee
Ajib alifunga bao pekee na la ushindi kwa kichwa dakika ya 36 akimalizia mpira uliopigwa na beki Kelvin Yondani aliyekuwa amesogea eneo la kati ya uwanja ili kupandisha mashambulizi.
Ndanda walijaribu kufika mara kadhaa langoni kwa Yanga kipindi cha kwanza lakini safu yao ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Omari Mponda na Nassor Kapama ilishindwa kupenya ngome ya Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’.
Kocha wa Ndanda Malale Hamsin aliwaingiza Kelvin Friday na Ophen Fransis kuchukua nafasi za Rajab Zahir na Kapama ili kuongeza kasi katika idara ya ushambuliajj lakini walishindwa kubadili matokeo.
Mwamuzi Jonesia Rukyaa kutoka mkoani Kagera aliwaonya kwa kuwaonyesha kadi ya njano Pappy Tshishimbi na  Raphael Daud wa Yanga na Jacob Masawe wa Ndanda kutokana na mchezo usio wa kiungwana.
Yanga imefikisha pointi nane ambapo sasa imewakuta watani wao wajadi Simba ambao juzi ilibanwa mbavu na Mbao FC kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment