Pages

Friday, September 15, 2017

TFF YATOA UTARATIBU WA MAWASILIANO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lingependa kutoa maelekezo ya kufuatwa kwa utaratibu wa mawasiliano kwa mfumo wa halakia  yaani ngazi moja baada ya nyingine kwa ukubwa.
Mawasiliano hayo yanalenga zaidi katika kualika viongozi wa kitaifa wa TFF katika programu au shughuli mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

TFF ingependa kuelekeza kuwa kama kuna suala la mwaliko au barua ya kwenda viongozi wa juu kuanzia kwa wadau, ngazi ya wilaya na mkoa kupita hatua moja baada ya nyingine kabla ya kufika katika ofisi ya Katibu Mkuu.

Tungependa kwa pamoja tushirikiane kwa kuheshimu mamlaka za mpira wa miguu zilizoko kwenye maeneo husika badala ya kufanya mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi juu.

No comments:

Post a Comment