Pages

Friday, September 1, 2017

MAYANGA AAHIDI USHINDI KESHO, KINDA LA BARCELONA LIKIONYESHA UFUNDI



MTANZANIA Abdulnasir Aziz anayecheza soka kwenye kituo cha Barcelona ya Hispania anatarajiwa kushuka kwenye dimba la Uhuru Dar es Salaam kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Botswana leo.
Abdulnasir yupo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na amefanya mazoezi tangu jana na leo na kocha Mayanga alisema anatarajia kumtumia kwenye mchezo wa kesho.
“Abdulnasir anacheza Barcelona kwenye timu ya watoto lakini kwa sasa yupo mapumziko na nimemwogeza katika kikosi na kesho nitamtumia kwenye mechi kwani amefanya mazoezi na wenzake,” alisema Mayanga.
Abdulnasir yupo kwenye program ya Aspire alijiunga Barcelona Februari mwaka huu akitokea akademi ya Dream Afrika.
Pia Mayanga alisema ameandaa kikosi chake vizuri kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi hivyo anatarajia kuendeleza rekodi ya kuifunga Botswana.
 “Botswana nilicheza nao na ulikuwa mchezo wangu wa kwanza tangu niteuliwe kuingoza Taifa Stars na niliwafunga mabao 2-0 na safari hii lazima tuwafunge tena,” alisema Mayanga aliyeteuliwa Januri 4
Pia Mayanga alisema kufanya vizuri kwa Taifa Stars inasaidia kuwatangaza wachezaji nje ya nchi na nchi kupanda kwenye viwango vya ubora vya FIFA ambavyo hutolewa kila mwezi.
Mayanga ameingoza Taifa Stars kwenye michezo 10 tangu aanze kuwa kocha wa timu hiyo na amefungwa mchezo mmoja,  sare minne na kushinda mitano.
Michezo hiyo na Matokeo yake ni dhidi ya Botswana 2-0, Burundi 2-1, Malawi 2-0, Mauritius 1-1, Angola 0-0, Afrika Kusini 1-0, Zambia ikashinda 4-2, Lesotho 4-3, Rwanda 1-1 na 0-0.
Naye kocha wa Botswana David Bright alisema kikosi chake kimechoka na walianza mazoezi jumatatu kwani wachezaji walikuwa kwenye timu zao lakini hatarajii kupoteza mchezo huu.
Kikosi cha Taifa Stars ni magolikipa; Aishi Manula, Mwadini Ally na Ramadhani Kabwili
Mabeki; Gardiel Michael,  Kelvin Yondan, Boniface Maganga, Abdi Banda, Salim Mbonde na Erasto Nyoni.
Viungo ni Himid Mao Hamisi Abdalla, Muzamiru Yassin, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Simon Msuva, Farid Mussa na Abdulnasir Aziz.
Washambuliaji ni Raphael Daud, Kelvin Sabato, Mbwana Samatta  na Elius Maguli.

No comments:

Post a Comment