Pages

Tuesday, September 19, 2017

LIGI DARAJA LA PILI KUANZA SEPTEMBA 30



LIGI Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL), inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana katika viwanja vitano tofauti.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema michezo itakayochezwa siku hiyo Kundi A ni kati ya Abajalo na Cosmopolitan, Namungo na Reha kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini.
Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkinafaso na Ihefu, Boma itacheza na Mkamba Rangers huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Mirambo.
Mchezo kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye Uwanja huo huo.
Lucas alisema sababu za mabadiliko haya yanatokana na kuwepo kwa mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC ambao utachezwa Septemba 30 katika uwanja huo.
Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.


No comments:

Post a Comment