Pages

Wednesday, September 27, 2017

HUYU NDIYE KOCHA WA MBEYA CITY

Image result for Nsanzurwimo Ramadhan
KOCHA Nsanzurwimo  Ramadhan amesaini makubaliano ya mwaka mmoja kuifundisha Mbeya City kwa mwaka mmoja.
Akizungumza Ofisa habari wa Mbeya City Shah Mjanja alisema uongozi wa Mbeya City umefikia makubaliano ya awali na Nsanzurwimo kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo kwa msimu mmoja.
“Kocha tayari yupo nchini na anatarajia kujiunga na timu huko kanda ya ziwa ambako inaendelea na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Mjanja
Nsanzurwimo raia wa Burundi amewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa kwa muda lakini pia amewahi kufundisha soka katika klabu kubwa za nchini Burundi, Rwanda, Botswana, Afrika Kusini, Malawi na Uganda.
Mbeya City ilivunja mkataba na kocha Mmalawi, Kinna Phiri mapema mwezi huu na kukubali kumlipa stahili zake kwa awamu.

Kwasasa Mbeya City ina pointi sita baada ya kucheza michezo minne na inashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment