Pages

Wednesday, September 6, 2017

BONGO MUVI YAUNGANA NA MAGUFULI KWENYE UZALENDO KWANZA









WASANII wa bongo muvi wameomba Watanzania kununua kama zao kwani wamejua walipokosea na sasa wamejirekebisha.
Hayo yalisemwa jana na Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere wakati wa kuzindua kampeni ya Uzalendo Kwanza ambayo itafanyika nchi nzima.
Steve alisema kampeni hiyo ni maalumu kuumunga mkono Rais wa Jamhuri wa Tanzania, John Magufuli ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhimiza uzalendo ikiwa ni pamoja na kulipa kodi kwa kudai risiti unapofanya malipo.
“Kampeni ya Uzalendo Kwanza itazunguka nchi nzima kwa ajili ya kuahamasisha Watanzania wote kuipenda nchi yao na kutunza raslimali zilizopo ikiwa ni pamoja na kununua kazi zinazozalishwa na Watanzania wenyewe,”
“Sisi wasanii wa filamu tunawaomba Watanzania wanunue kazi zetu kwani tumejua tulipokosea na tumebadilika na kwa kufanya hivyo tunasaidia kuingiza kipato kwa nchi kwani tunalipa kodi kupitia stampu iliyopo kwenye kasha,” alisema Steve.
Pia alisema Tanzania inawadai hivyo ni muhimu wakaunangisha nguvu kulinda Amani na kulinda raslimali za nchi na kuahidi kutoa kazi nzuri.
Naye msanii mkongwe Bibi Mwenda aliwaasa wazazi kuwafundisha watoto kuwa wazaqlendo kwani wamezaliwa Tanzania na Tanzania ndio nchi yao.
“Utamsikia mtoto anasema Bongo bahati mbaya na wewe mzazi unanyamaza, hiyo haipendezi, Tanzania ni nchi yetu lazima tuipende,” alisema Bibi Mwenda

No comments:

Post a Comment