Pages

Friday, August 25, 2017

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO VIJANA KINONDONI


Mabondia Baina Mazola kushoto akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao kesho katika ukumbi wa Vijana Kinondoni
Mratibu wa mpambano wa masumbwi kaizirege Dragon Kaizum katikati akiwatambulisha mabondia mbele ya wahandishi wa habari kushoto ni Baina Mazola na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa agost 26 jumamosi hii litakalofanyika katika ukumbi wa vijana kinondoni 
Bondia Selemani Simba akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Kallage Hassani utakaofanyika kesho katika ukumbi wa vijana kinondoni

Mabondia Kallage Hassani kushoto akitunishiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni

Mabondia Kallage Hassani kushoto akituniashiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni


Mabondia Cosmas Cheka Kushoto akitambiana na Haidal Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni 

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Baina Mazola 'Simba Mazola' na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  wamepia uzito kwa ajili ya mpambano wao  utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mpambano wa raundi nane uzito wa kg 57

Wakiongea kwa nyakati tofauti kambi hizo zimejigamba kila mmoja kumpiga mwenzake raundi za awali

Kwa upande wa Miyeyusho amejigamba kuwa katika mabondia wa Mabibo wanaofundishwa na kocha Cristopher Mzazi akuna anayemsumbua hata mmoja hii ni pambano la kisasi ukumbuke kuwa Mzazi ana mabondia wengi na mimi ndie ninayemharibia


Kwa upande wa Mazola nae ametamba kumsambaratisha mpinzani wake raundi za mwanzo kwani hana jipya ukumbuke mchezo wa ngumi sio sawa na michezo mingine umri ukienda biashara imekwisha sasa anaenda kumstaafisha rasmi hivyo wapenzi waje kwa wingi ili waone anavyo mwachisha ngumi

Nae mratibu wa mpambano huo kaizirege Dragon Kaizum amesema mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakati bondia kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' atakumbana na Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashidi Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini

No comments:

Post a Comment