Pages

Friday, August 25, 2017

INFANTINO AMPONGEZA KARIA, AMKARIBISHA ZURICH



RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino na chama cha soka Rwanda, wametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa Rais kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya 2017-2021.

Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema, Infantino katika barua yake ya Agosti 14, 2017 alimpongezi Karia na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake na kusema hana shaka na uwezo wake.

“Kwa wakati wote, nakuhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka FIFA katika malengo yako na milango iko wazi wakati wote wewe kuja kujadili masuala ya mchezo wa mpira wa miguu hasa eneo la utawala.

“Nimeagiza upande wa utawala kuwasiliana nawe kuona na kupanga tarehe rasmi ya safari, nikutakie kheri na fanaka, nguvu na kila aina ya mafanikio katika majukumu yako mapya huku nikitarajia ujio wa kuonana nawe haraka,” alisema

Pia barua hiyo inasema Infantino hana hana shaka na uwezo wa Karia ukizingatia alikuwa Makamu wa Rais wa kipindi kilichopita, hivyo atakuwa fursa ya kuiletea nchi maendeleo ya mchezo soka.

Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda (FERWAFA) nalo kwa upande wake wamempongeza Rais wa TFF, Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa kiongozi mpya wa shirikisho. 

Wakati huo huo Rais wa shirikisho la Rwanda, (FERWAFA) Nzamwita Vincent imesema Rwanda itaendelea kuwa bega kwa bega na Tanzania katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa ushirikiano baina ya nchi mbili za ukanda wa Afrika Mashariki unaounda Baraza la Soka la nchi za Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment