Pages

Tuesday, August 29, 2017

CLEMENT SANGA WA YANGA NA HAMAD JUMA WAPITISHWA KUGOMBEA KAMATI YA BODI YA LIGI



KAIMU Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na Hamad Juma wamepitishwa kugombea uenyekiti wa kamati ya Bodi ya Ligi Tanzania katika mchujo wa awali.
Akizungumza na wadishi wa habari, Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas alisema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 15, Dar es Salaam.
“Nafasi zitakazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watatu kuwakilisha klabu za Ligi (PL), Wajumbe wawili wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Mjumbe mmoja wa kuwakilisha klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL),” alisema Lucas.
Katika nafasi ya makamu mwenyekiti ina mgombea mmoja ambaye ni Shani Christoms na kwenye ujumbe wa timu za ligi kuu ni wawili pekee waliopitishwa wakati nafasi hiyo inahitaji wagombea watatu.
Waliopitishwa ni Hamis Madaki na Ramadhan Mahano na wajumbe wa timu za ligi daraja la pili wwaliopitishwa ni Almas Kasongo na James Bwire na daraja la pili ni Edgar Chibura.
Uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

No comments:

Post a Comment