SHAFIIH DAUDA ATANGAZA KUJITOA KWENYE UCHAGUZI TFF
MGOMBEA wa
kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kutoka kanda ya Dar es
Salaam, Shaffih Dauda amejitoa
Akizungumza
kupitia kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Clouds ambapo
pia yeye ni mtangazaji Shaffih alisema amefikia hatua hiyo baada ya kuona mbinu
na siasa chafu zinazoendeshwa juu yake.
“Mimi ni
mfanyakazi wa Clouds Media Group nilikwenda Mwanza kwa ajili ya kazi. Hapa
Clouds tumelelewa kufanya kazi kwa bidii kufikia malengo hivyo sitaki mambo
yangu binafsi (kugombea uongozi TFF) kuharibu malengo ya mashindano ya Ndondo na taasisi
yangu,” alisema Shaffih
“Nimeangaika
kutengeneza jina langu kwa miaka mingi. Natangaza kujitoa rasmi kugombea,
nitaendelea kuchangia kwenye maendeleo ya soka nikiwa sio kiongozi,” alisema
Shaffih.
Pamoja na kuwa alikuwa anagombea ujumbe wa kamati ya Utendaji TFF pia ni mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Chama cha soka mkoa wa Ubungo (UFA) ni kiongozi pia.
Kauli ya
Shaffih kujitoa imekuja ikiwa ni siku nne tangu akamatwe na Taasisi ya Kuzuia
na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa
wa Mwanza kwa tuhuma za rushwa pamoja na viongozi wengine wa soka kumi.
Hata hivyo
kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana leo kwa ajili ya kutangaza orodha ya mwisho
ya wagombea wa nafasi mbalimbali wa uchaguzi wa TFF ambao wataanza kampeni
Agosti 5.
Post a Comment