Pages

Wednesday, June 21, 2017

USAJILI WA MBARAKA SARAKASI TUPU



 Image result for MBARAKA YUSUPH IMAGES
SAKATA la mkataba wa mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph ambaye amesajiliwa na Azam FC msimu huu limeingia katika sura mpya baada ya mchezaji huyo kwenda katika Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchukua nakala ya mkataba wake wa zamani na kupewa mikataba miwili tofauti.
Akizungumza Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed alisema kabla ya kuingia makubaliano ya kusaini mkataba na Mbaraka walijiridhisha kuwa hana mkataba na Kagera lakini wameshangaa baada ya kwenda TFF na kupewa mikataba miwili tofauti


 “Sisi Azam FC tulikuwa na nakala halisi ambayo iliwasilishwa TFF kwenye usajili ulikwish lakini tulimwambia Mbaraka akachukue nakala yake TFF, ajabu amepatiwa nakala mbili tofauti,”.
“Nakala moja inaonyesha mkataba uliosainiwa ni wa mwaka mmoja ambao ulisainiwa Juni 20, 2016 na mwingine unaonyesha ni wa miaka mitatu ambao umesainiwa Agosti 10, 2016,” alisema Abdul
Pia Abdul alisema ukiacha tofauti ya miezi mitatu ya kusainiwa mikataba hii, lakini hata kiwango cha usajili ni tofauti mno kwani mkataba wa miaka mitatu hauna saini ya mchezaji, wala muhuri wa Kagera Sugar na jina la mchezaji kwenye sehemu ya kusaini halijaandikwa.
Aidha Abdul alisema wataiweka hadharani mikataba  hiyo endapo mchezaji Mbaraka ataridhia ili familia ya soka ione mikataba yote miwili na kisha tarataibu nyingine zifuate kwani kuna uhuni mwingi ambao unafanywa kwenye baadhi ya mambo, hasa masuala ya mikataba ya wachezaji.
”Sisi Azam tunataka kulimaliza tatizo hili. Na kwa hili tutatumia wanasheria wetu kuwafikisha mahakamani wote walioshiriki kufoji mkataba wa Mbaraka ili kujenga precedent nzuri huko mbele,” alisema Abdul
Abdul aliwataka uongozi wa Kagera Sugar kukanusha au kuthibitisha juu ya mikataba hii ili hatua stahiki ziweze kufuatwa kwani suala la kufoji mikataba ya wachezaji ni uhuni ambao haupaswi kuachwa kuendelea kwenye mpira.


No comments:

Post a Comment