Pages

Saturday, June 17, 2017

UCHAGUZI WA TFF KAZI IMEANZA, WAJUMBE WAPISHANA KUCHUKUA FOMU




RAIS Jamal Malinzi amechukua fomu kutetea kiti chake katika uchaguzi Mkuu  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  leo Dar es Salaam.
Wengine waliochukua fomu za kuwania Urais ni Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Madega, Makamu wa Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas waliochukua fomu za kuomba Umakamu wa Rais ni Mulamu Nghambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambao wanachama wa klabu ya Simba. Kaburu ni Makamu wa Rais wa Simba kwa sasa.
Nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Salum Chama, Ephraim Majige, Elias Mwanjala, Saleh Alawi, Kaliro Samson, Vedastus Lufano, Kenneth Pesambili, Mbasha Matutu, Samuel Daniel, Dunstan Mkundi, Athumani Kambi, Shaffi Dauda, Golden Sanga, Charles Mwakambaya, Benista Rugola, Thabit Kandoro, Goodluck Moshi, James Mhagama, Hussein Mwamba, Sarah Chao, Issa Bukuku, Stewart Masima, Emmanuel Ashery, Abdul Sauko, Mussa Sima, Stanslaus Nyongo, Ayoub Nyenzi, John Kadutu, Baraka Mazengo, Khalid Mohamed, Mohamed Aden, Cyprian Kuyava na Saleh Abdul.
Uchaguzi Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma wakati zoezi la kuchukua fomu litakamilika Juni 20, mwaka huu na kikao cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mkapa Juni 23.
Juni 24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa siku za kupokea na kuweka mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka Julai Mosi itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi yote na kufanya usaili.
Kwa mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika matokeo ya usaili, Julai 4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha masuala ya Kimaadili kwenye Kamati ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya kimaadili.
Julai 15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya  masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa siku ya kusikiliza rufaa za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29 mpaka Agosti 2.
Wagombea watajulishwa matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa siku ya kuchapisha majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo na kampeni kwa wagombea zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata yaani Agosti 12 itakuwa siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.
Nafasi zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita; Mara na Mwanza; Shinyanga na Simiyu; Arusha na Manyara; Kigoma na Tabora; Katavi na Rukwa; Mbeya na Iringa; Njombe na Ruvuma; Lindi na Mtwara; Dodoma na Singida; Pwani na Morogoro; Kilimanjaro na Tanga na Kanda maalum ya Dar es Salaam.
Fomu za Urais zinapatikana kwa Sh. 500,000, Makamu wa Rais Sh. 300,000 na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Sh. 200,000.

No comments:

Post a Comment