Pages

Wednesday, June 21, 2017

KAUZU YAMALIZA UBISHI KWA SHERATON



KAUZU imemaliza vita ya majirani wa Temeke baada ya kuifunga Sheraton FC mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa jana katika Uwanja wa Tandika Mabatini, Temeke
Timu hizi majirani kama ilivyo Liverpool na Everton za England zina ushindani lakini Kauzu walipata bao la kwanza dakika ya tano lililofungwa na Hamad Kibopile.
Kama haitoshi dakika 23 Kauzu wakapata bao lao la pili lililofungwa na Awadh Said na kwenda mapumziko Kauzu wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Sheraton walicharuka na kufanikiwa kufunga bao dakika ya 56 ambalo lilidumu hadi dakika 90.
Kauzu wanaongoza Kundi H wakiwa na pointi tatu wakifuatiwa na Faru Jeuri na Miami ambao wote wana pointi mojamoja huku Sheratoni wakiwa mkiani  bila pointi.
Katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Ilala Faru Jeuri walitoshana nguvu na Miami baada ya kutoka suluhu.

No comments:

Post a Comment