Pages

Saturday, June 10, 2017

Hakuna kulipwa Kombe la Dunia la vijana



Timu za Taifa za Vijana walio chini ya umri wa miaka 20 za Uingereza na Venezuela kesho zitapambana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la vijana nchini Korea Kusini.
Timu hizo zitacheza kwa ajili ya kombe, medali na uzalendo tu baada ya kufahamika kuwa hakuna zawadi ya malipo yoyote kutoka katika Shirikisho la Soka Duniani, FIFA katika michuano ya Kombe la Dunia ya vijana walio chini ya umri wa miaka 20.
Kama vile haitoshi, hakuna malipo ya ada ya ushiriki, marupurupu wala bonasi kwa wachezaji hao vijana kama ilivyo katika michuano ya wakubwa ambayo huwa na malipo makubwa kwa wachezaji na zawadi za ubingwa.

No comments:

Post a Comment