WAKATI Real
Madrid wakijiandaa kuumana na Juventus kwenye fainali ya kukata na shoka ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) Jumamosi hii nyumbani kwa Gareth Bale jijini
Cardiff, mchezaji huyo ameng’aka na kusema hali ni mbaya na UCL haijapata kuacha
waliomo salama.
Bale
aliyepata kuwa mchezaji ghali zaidi duniani, akiuzwa Madrid kutoka Tottenham
Hotspur kabla ya kuja kuzidiwa na Paul Pogba aliyeuzwa kwa pauni milioni 89
kutoka huko Juventus kwenda Manchester United, anasema anapiga hesabu jinsi ya
kuwamaliza Wataliano hao.
Nyota wa
Madrid wanajifua, wakiamini kwamba watafanya vyema, hasa baada ya Bale
aliyekuwa majeruhi kurejea uwanjani, japokuwa mwenyewe anasema kwamba hajakuwa
timamu kwa asilimia 100. Anatarajiwa kuungisha nguvu pale mbele na Cristiano
Ronaldo na Karim Benzema.
Japokuwa
atakuwa anacheza jijini kwake Cardiff, Bale anasema mambo hayo ufanye kuyasikia
tu kwa watu lakini ukishaingia ndani mwake, kuna kuachwa mpauko au kushinda, na
hakuna kubaki bila upande – ni kupiga au kupigwa tu.
Upo
uwezekano mkubwa kwa mchezaji huyu wa kimataifa wa Wales kuanzia benchi lakini
akaingia baada ya muda, akiwa ameanza mechi 23 kwenye mashindano yote msimu
huu. Kocha Zinedine Zidane hana shaka kwamba ataweza kupanga watu wanaoweza
kumpa matokeo chanya kwenye mechi hiyo.
“Sipo timamu
kwa asilimia 100, nimecheza kwa wiki sita au saba tu. Kudumu dimbani kwa dakika
90 ni ngumu kwangu kwa sababu sijacheza sana soka tangu nilipofanyiwa upasuaji
na kuna wakati nilicheza na maumivu makubwa na hata niliporejea nilikuwa nameza
dawa. Wiki chache zilizopita zimeniwezesha kupumzisha enka yangu kwa muda,”
anasema Bale.
No comments:
Post a Comment