Ivan 39, alikuwa amelazwa katika hospitali ya Steve Biko iliyopo katika jijini la Pretoria nchini Afrika Kusini kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo kabla ya kuaga dunia.
Ivan amezaa na mrembo huyo watoto watatu wa kiume kabla ya kutengana ambapo Zari alianza mahusiano na msanii nyota wa muziki wa Bongo fleva Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ ambaye amezaa nae watoto wawili.
Katika siku chache zilizopita kulikuwa na taarifa za kuugua ghafla kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini Uganda ambaye pia ni miongoni mwa vijana wenye pesa nyingi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram mapema asubuhi ya leo Zari aliandika ujumbe wa kuomboleza msiba huo huku akisema Ivan alikuwa bado ni muhimu hasa katika ustawi wa watoto wao watatu wa kiume.
Zari aliandika pia kwenye ukurasa wa Instagram siku chache zilizopita akimtakia kheri ya kupona haraka kutokana na maradhi hayo ambayo yamepelekea kifo chake.
No comments:
Post a Comment