SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limeteua makocha 26 kwa ajili ya kufanya skauti za vijana wenye vipaji vya soka kwenye
mashindano ya shule za msingi (Umitashumta) na Sekondari (Umisseta) ngazi za
mikoa watakaojumuishwa kwa maandalizi ya
michuano ya Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum
Madadi alisema TFF kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imedhamiria kuboresha mashindano hayo ili kupata
vijana wengi wenye vipaji kuanzia ngazi
ya mkoa na Taifa.
Mashindano
ya Umisseta ngazi ya taifa yanatarajiwa kufanyika Juni 6 hadi 17 na Umitashumta
Juni 27 hadi 28 jijini Mwanza ambapo mikoa itapeleka timu zao kuwakilisha
kitaifa.
“Tumejipanga kwenda kuchagua vijana ngazi ya
mkoa na baadaye kitaifa. Tunategemea makocha tuliowateua watatufanyia kazi hiyo
kutoka kila mkoa na baadaye kutakuwa na jopo la makocha sita watakaokuwa Mwanza
kwenye fainali Umitashumta na Umisseta,”alisema.
Alisema
wanataka kuibua vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 13 ambao
watashiriki fainali za mataifa ya Afrika
chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2021. Hivyo maandalizi yaanza kuanzia sasa.
Pia, alisema
wataboresha kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 15 watakaoshiriki fainali
za vijana chini ya umri wa miaka 17, mwaka 2019. Lakini pia, watachaguliwa
vijana chini ya umri wa miaka 20 kuboresha kikosi hicho cha Ngorongoro Heroes.
Makocha
walioteuliwa mikoa mbalimbali ni Oscar Mirambo (DSM), Kessy Mziray (Mwanza),
Shaweji Nawanda (Mtwara), Charles Mayaya (Shinyanga), Mohamed Muya (Dodoma),
Mohamed Laizer (Arusha), Madenge Omari (Mara),Samwel Moja (Lindi), Issa Mgaza
(Kilimanjaro), Khamis Mambo (Kigoma), John Nzongwe (Geita), Zakaria Mwamba
(Rukwa), Godfrey Mvula (Ruvuma) na Aloyce Mayombo (Pwani),
Wengine ni Osuri Kosori (Simiyu), Gabriel Gunda (Singida) Zahoro Ramadhan (Tanga),
Athuman Kairo (Morogoro), Fidelis Kalinga (Iringa), Ally Kagire (Kagera),
Mohamed Bachoro (Katavi), Albeti Gama (Njombe), Andrew Nzoma (Tabora), Anthony
Mwamlima (Songwe), Gaul Msalia (Mbeya) na Victor Kijazi (Manyara).
No comments:
Post a Comment