Pages
▼
Monday, May 29, 2017
SIMBA NA SHANGWE ZA UBNGWA WA SHIRIKISHO
BAO la mkwaju wa penati dakika za lala salama la winga Shiza Kichuya ulitosha kuipa Simba ubingwa wa kombe la FA baada ya kuifunga Mbao FC mabao 2-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mtanange huo ulilazimika kwenda katika muda wa nyongeza baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bila kufungana.
Mchezo huo ulianza taratibu huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini Simba walitawala sehemu kubwa ya mchezo huku mshambuliaji Laudit Mavugo akipoteza nafasi mbili za kufunga kipindi cha kwanza.
Simba walitumia zaidi mipira mirefu kutokana na nyasi za uwanja wa Jamhuri kutokuwa rafiki kwa pasi za chini kama walivyozoea katika uwanja wa Taifa japokuwa mabeki wa kati wa Mbao Yusuph Ndikumana na Asante Kwasi walikuwa imara kuondoa hatari zote.
Kipindi cha pili kilianza kwa kosa kosa kwa timu zote lakini safu za ulinzi zilifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari.
Blagnon alifunga bao dakika ya 95 kufuatia mpira mrefu kutoka nyuma uliopigwa na beki Abdi Banda lakini Ndaki Robert aliisawazishia Mbao dakika nane baadae na kupelekea mchezo huo uende katika muda wa ziada.
Kocha wa Simba Joseph aliwatoa Mohammed Hussein, Juma Liuzio na Said Ndemla na kuwaingiza Abdi Banda, Ibrahim Ajib na Blagnon wakati Mbao ikimpumzisha George Sangija nafasi yake ikachukuliwa na Dickson Ambundo.
James Kotei wa Simba amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa fainali huku Obrey Chirwa akiibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao sita.
No comments:
Post a Comment