WAZIRI wa
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk.Harisson Mwakyembe amewataka
wachezaji wa timu ya Taifa ya Wachezaji wa chini ya miaka 17, Serengeti
kutokata tamaa badala yake kujipanga kuitumikia timu ya U-20.
Dk. Mwakyembe
alisema hayo baada ya kuipokea timu hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Nyerere iliporejea kutokea nchini Gabon ilipokuwa ikishiriki michuano
ya Kombe la Mataifa Afrika la U-17.
Timu hiyo
ambayo imetolewa ikiwa inashikiria nafasi ya pili baada ya kufungwa 1-0 na
Niger na hivyo kulazimika kuyaaga mashindano hayo kwa kanuni ya head to head
Mwakyembe
alisema Serengeti imewakilisha vema nchi kwa kushiriki kwao kwenye michuano
hiyo kwa kuwa mara ya mwisho kwa nchi kuingia hatua hiyo ni miaka 37 iliyopita.
Alisema,
watanzania wanatambua kazi ngumu ambayo timu hiyo imefanya na hasa kwa kushinda
baadhi ya michezo yake ikiwa ni pamoja na kutoa sare dhidi ya Mali ambao ni
mabingwa watetezi.
"Nyie
ni washindi kwa kuwa asiekubali kushindwa sio mshindani na nyie ni washindi kwa
kuwa mlichokifanya sio cha kawaida, na hata hao Niger wameshinda ni kama
wamebahatisha tu Wizara ipo nanyi na tutawaendeleza".
Aliongeza"
nilikuwa bungeni Dodoma, na nimemuomba ruhusa Mheshimiwa Spika ili aniruhusu
nije kuungana na nyinyi na sasa tusilie ila tujipange".
Aliuomba
uongozi wa timu hiyo kuipeleka mkoani Dodoma kwa ajilia ya mchezo wa kirafiki
na wabunge ikiwa ni sehemu ya kuwaonesha uwezo wao kisoka.
Aliongeza, huku
wachezaji hao wakianza kambi kwa ajili ya kuiwakilisha Ngorongoro tayari
maandalizi ya kuiinua itakayokuwa Serengeti yameanza.
Kwa upande
wake Mkuu wa msafara, Ayoub Nyenzi alishindwa kuvumilia na kujikuta akiangusha
kilio wakati akizungumzia michuano hiyo ilivyokuwa chini Gabon.
Wachezaji
waliwasili majira ya saa nane unusu na baada ya kuwasili ilienda moja kwa moja
kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya kuwapokea ndani ya Uwanja huo.
Walikabidhiwa
maua huku Waziri Mwakyembe akiwa na jukumu la kuwapokea katika lango la
kuelekea kwenye eneo hilo na alisikika akiwafariji wachezaji hao.
Nje ya eneo
la Uwanja kulikuwapo na wazazi, ndugu na jamaa wa wachezaji hao walioenda
kuwasalimia kabla ya wachezaji hao hawajapanda basi lao kuelekea kambini.
No comments:
Post a Comment