KESHO timu
ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’ wanatarajiwa kutupa
karata yao ya kwanza katika fainali za 12 za mashindano ya Afrika zinazofanyika
nchini Gabon kuanzia leo.
Serengeti
boys ambayo tayari wapo Gabon tangu Mei 7 zitakuwa fainali zitakuwa fainali zao
za kwanza huku watanzania wakiweka
matumaini makubwa kwao pengine wanaweza kututoa kimasomaso.
Kikosi hiki
cha Serengeti boys kimeandaliwa kuleta ushindani kwani kimecheza michezo saba
ya kirafiki ya kimataifa, kati hizo imeshinda michezo mitano, sare mmoja na
kufungwa mmoja.
Tanzania
itakuwa na wachezaji 21 ambao wamepitishwa na Shirikisho la soka barani Afrika
(CAF) ambazo zitakuwa fainali za 12 toka kuanzishwa kwa michuano hiyo ambapo
tamati yake itakuwa Mei 28.
Timu shiriki
zimegawanywa katika makundi mawili; kundi A lina timu za wenyeji Gabon, Guinea,
Cameroon na Ghana na kundi B lina timu za Tanzania, Mali, Niger na Angola
Kundi A ndilo linafungua dimba leo ambapo wenyeji Gabon wanacheza
na Guinea ikifuatiwa na Cameroun ambaye ataoneshana ubabe na Ghana mjini Port Gentil.
Kundi B, litaanza kutupa karata zao kesho ambapo Serengeti boys
itafungua dimba na bingwa mtetezi Mali , kwenye Uwanja wa Franceville, Libreville na
kufuatiwa na mchezo wa Angola dhidi ya Niger.
Mchezo huo
utachezwa saa 9:00 za Gabon ambapo ni sawa na saa 12:00 za Tanzania.
Mchezo wa
pili utakuwa dhidi ya Niger Mei 18 saa 9:00 za Gabon sawa na saa 12:00 za
Tanzania
Mchezo wa
mwisho kwenye makundi itacheza na Angola, Mei 21 saa 2:00 mbili usiku sawa na
5:00 usiku za Tanzania.
Timu zitakazofuzu
nusu fainali zitakuwa zimefuzu kuwakilisha
Afrika katika fainali za FIFA U-17 zitakazofanyika nchini India kuanzia Oktoba
06-28, 2017.
Katika kuhakikisha
Serengeti boys inafanya vizuri wadau mbalimbali wamejitokeza kuichangia timu
hiyo ambayo ni mara ya kwanza kushiriki baada ya kufuzu na kuondolewa baada ya
kumchezesha Nurdin Bakari ambaye alikuwa amezidi umri.
Serengeti boys ni timu
pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo ilifuzu baada ya kutolewa kwa
Congo Brazaville iliyomchezesha mchezaji aliyezidi umri.
Kocha wa Serengeti boys, Bakari Shime wamefanya maandalizi mazuri
ambayo yanaifanya timu yake kuwa tayari kwa mashindano na lengo lao ni kubaki
katika nne bora ili kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika India.
“Tuko tayari kwa
mashindano.Mipango yetu inakwenda vizuri na tumecheza mechi saba ambazo
zimeonesha maendeleo. Tunatarajia mashindano magumu lakini tutapambana ili
kufikia malengo yetu, “alisema Shime.
“Ari ya wachezaji iko
juu.Sasatunaweza kusema kuwa tuko tayari kwa mashindano na tunawaomba
Watanzania kutuunga mkono.”alisema Shime
Serengeti boys ilipiga kambi Morocco kwa takribani siku 21, ambapo
ilicheza na Gabon katika mechi mbili za kirafiki, ambapo ilishinda 2-1 katika
kila mchezo.
Kambi ya mwisho ilikuwa Yaounde, katika mji mkuu wa Cameroon,
ambako timu ilipumzika kwa siku nane. Serengeti iliwashtua wenyeji kwa kuifunga
1-0 katika mchezo wa kwanza kabla ya kupoteza kwa idadi hiyo ya bao katika
mchezo wa marudiano.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu kabla Serengeti boys kuondoka Morocco
kuweka kambi aliiandalia chakula cha jioni huku akiwaasa wachezaji hao kupigana
kufa na kupona kwani watanzania wanapenda kusikia wanafanya vizuri.
Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiongoza harambee ya
kuichangia timu hiyo hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF)
alisema wana imani na Serengeti boys kuwa inakwenda kufanya vizuri na
kuichangia shilingi milioni tano.
Wadau mbalimbali na vyama vingine vya michezo vimetoa salamu
nyingi kuitakia heri Serengeti boys ambayo Jumatatu itakuwa Uwanjani kumenyana
na bingwa mtetezi, Mali.
Katika kuonesha
kila kitu kipo tayari Shirikisho la Soka barani Afrika limepitisha orodha ya
wachezaji 21 kwa kila timu ambazo zinashiriki fainali hizo.
Yafuatayo ni
majina 21 ya wachezaji wa Serengeti boys waliopitishwa na nafasi watakazokuwa
wanacheza na mwaka aliozaliwa .
Kikosi cha
Serengeti boys kilichopitishwa ni makipa
Ramadhan
Kabwili, Samwel Edward, Kelvin Kayego:
Mabeki ni Enrick
Vitalis, Dickson Job, Issa Makamba, Ally Msengi Nickson Kibabage
Viungo ni
Kelvin Nashon, Shaaban Ada, Cyprian Benedictor, Saidi Mussa, Ally Ng’anzi
Washambuliaji:Yohana
Mkomola, Muhsin Malima, Ibrahim Abdallah. Israel Mwenda, Kibwana Ally, Mohamed
Rashid, Assad Juma ,Abdul Suleiman
No comments:
Post a Comment