RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal
Malinzi ameondoa utata na mabishano ya
mashabiki wa soka nchini juu ya nani atapata zawadi ya mfungaji bora baada ya
wachezaji wawili kufungana kwa idadi sawa ya mabao.
Wachezaji hao ni Simon Msuva wa Yanga na
Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, ambao kila mmoja amefanikiwa kutupia mabao 14.
Kwa mujibu wa Tweet ya Malinzi aliyotoa leo, wachezaji wote kwa kuwa wamelingana
idadi ya mabao, hivyo watapewa zawadi sawa.
“Kwa kuwa vijana wetu Mussa na Msuva wamefunga
mabao 14 wote ni wafungaji bora na watapewa zawadi sawa sh. Milioni
5.8,”alisema.
Mbali na wachezaji hao wanaowania tuzo ya mfungaji
bora, kutakuwa na tuzo nyingine ikiwemo
kikosi bora cha msimu, tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 20,
tuzo za bingwa wa Ligi Kuu, mshindi wa pili, wa tatu na nne.
Sherehe za utoaji tuzo zinatarajiwa kutolewa Mei
24, mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana
na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu: Aishi Manula – Azam,
Simon Msuva – Yanga, Shiza Kichuya – Simba, Haruna Niyonzima– Yanga, Mohammed Huseein
-Simba
Kipa bora: Aishi Manula– Azam, Owen Chaima –
Mbeya City, Juma Kaseja – Kagera Sugar.
Kocha Bora: Joseph Omog – Simba, Mecky Maxime –
Kagera Sugar, Ettiene Ndayiragije – Mbao.
Mmwamuzi bora : Shomari Lawi – Kigoma, Elly Sasii
– Dar es Salaam, Hance Mabena – Tanga
Mchezaji bora wa kigeni: Haruna Nyonzima –
Yanga, Method Mwanjale – Simba, Yusuph Ndikumana – Mbao
Mchezaji bora
anayechipukia : Mbaraka Abeid – Kagera Sugar, Shaaban Idd – Azam,
Mohammed Issa – Mtibwa.
Tuzo ya Ismail Khalifan (U-20): Shaaban Idd – Azam, Abdalah Masoud –
Azam, Mosses Kitambi – Simba.
Tuzo ya heshima: (Atatangazwa aliyeteuliwa siku
hiyohiyo ya sherehe za tuzo), goli bora la msimu: (Tayari yamepatikana mabao
bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima)
na timu yenye nidhamu (Mshindi atatangazwa ukumbini).
No comments:
Post a Comment