MANCHESTER,
England
WAYNE Rooney ana ofa mbili za pauni milioni 50 za
kujiunga na moja ya klabu za China akitokea Manchester United.
Lakini
inadhaniwa Rooney atapata wakati mgumu kukataa uwezekano wa kurejea kwenye
klabu iliyomkuza ya Everton pamoja na fedha nyingi kutoka klabu za China.
Maisha ya
mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwenye timu ya taifa ya England
yalikoma baada ya kocha wa timu hiyo Gareth Southgate kumuacha nje ya kikosi
chake na sasa inaelezwa anafikiria ofa ya pauni milioni 50 kutoka China, ambapo
hata kwa kiwango cha maisha ya Rooney bado hizo ni fedha nyingi.
Amejadili
uwezekano wa kuhamia China na familia yake na atafanya uamuzi juu ya hatima
yake wiki ijayo. Lakini ofa ya dakika za mwisho kutoka Everton inaweza
kumshawishi Rooney kubaki England.
Everton haiwezi kukaribia kiwango kikubwa cha fedha
ambacho China itampa Rooney, lakini mabosi wa klabu hiyo wamedhamiria
kumrejesha Rooney kwenye klabu hiyo ya tangu utoto wake.
Everton
itampa Rooney mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki kidogo zaidi ya mshahara
anaolipwa na Manchester United atapoachana na klabu hiyo aliyoshinda nayo
mataji 13. Mshahara wake kwa China utakuwa pauni 480,000 kwa wiki.
Rooney
alisema: “Kuna ofa nyingi mezani, kwa England na nje ya England na hakika hizo
ndizo natakiwa nizifanyie maamuzi.”
No comments:
Post a Comment