TANZANIA imepanda kwa nafasi 22 kwenye
viwango vya ubora wa soka kwa wanaume Machi kufuatia matokeo mazuri iliyoyapata
katika michezo ya kirafiki ya kimataifa hivi karibuni.
Februari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya
157 huku katika viwango vilivyotangazwa leo na FIFA ikikamata nafasi ya 135.
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
iliifunga Botswana mabao 2-0 kabla haijaibutua Burundi 2-1 mwishoni mwa mwezi
uliopita.
Brazil imeipiku Argentina katika nafasi ya
kwanza huku Ujerumani ikishika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment