Wachezaji wa Timu ya Serengeti Boys wakimpongeza mfungaji wao wa bao la pili Ibrahim Abdallah
2-0
TIMU ya Taifa ya soka ya Vijana waliochini ya miaka 17
‘Serengeti boys’kesho inashuka uwanjani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa
dhidi ya Ghana utakaochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo maalumu kwa ajili ya kuiaga timu hiyo ambayo
inakwenda kuweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kujianda na fainali za
Afrika za vijana, nchini Gabon unakuja ikiwa ni takribani siku nne tangu
iifunge timu ya taifa ya Burundi kwa mabao 5-0.
Serengeti boys ilicheza na Burundi kwenye Uwanja wa
Kaitaba Kagera na kufanikiwa kuifunga timu hiyo kwenye mchezo wa kwanza mabao
3-0 na mchezo wa pili uliochezwa juzi mabao 2-0.
Akizungumza jijini, Ofisa habari wa Shirikisho la
Soka Tanzania, (TFF), Alfred Lucas alisema Ghana ambao nao wanashiriki fainali
za vijana iliwasili nchini tangu Ijumaa usiku.
“Mchezo huu ndio vijana wetu wanaotumia kama sehemu ya
kuwaaga watanzania kwani tunatarajia kiongozi mzito wa serikali atakuwepo ili
kukabidhi bendera,” alisema Lucas.
Aprili 5, Serengeti boys inatarajiwa
kusafiri kwenda Morocco kwa ajili ya kambi na ikiwa Morocco itacheza michezo ya
kimataifa ya kirafiki na Cameroon na Misri na Mei 6 itakwenda Gabon tayari kwa
mashindano kwani wanatakiwa wawe wamewasili Mei 7.
Serengeti Boys imepangwa kundi ‘B’
pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola ambapo fainali hizo
zinajuisha mataifa nane ya Afrika, endapo Serengeti itafuzu nusu fainali
itakuwa imekata tiketi ya kucheza fainali za dunia za vijana zitakazofanyika
India, Novemba.
No comments:
Post a Comment