![https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzdoyOGMIYPavH2u92QjkTTk-lvV92o-Yfn_zjVIZxl-Jx64gWlObRJHnN1kf3cRA6sgdLajbTmvQ3LtJGjWeTlBzR3dPh0uhQewSETRnPMtCXKSZkRawyWgTrcitszEaQs8kcGbsWzIY/s1600/WhatsApp+Image+2017-03-16+at+1.25.02+PM.jpeg](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzdoyOGMIYPavH2u92QjkTTk-lvV92o-Yfn_zjVIZxl-Jx64gWlObRJHnN1kf3cRA6sgdLajbTmvQ3LtJGjWeTlBzR3dPh0uhQewSETRnPMtCXKSZkRawyWgTrcitszEaQs8kcGbsWzIY/s280/WhatsApp+Image+2017-03-16+at+1.25.02+PM.jpeg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjP8BhIO4JHJaRiy6Tf4sm__UpLm2sTSwiwbjWrxzUp6BSmVYibdETABOnU7MOJBQSz8bljNd-FxCMg1jMF6m3nx5S13uRu88k4hSwZl3-9iLysJnDxuNJO1IZYgrw4iEhTAIMKaUV0sHo/s280/WhatsApp+Image+2017-03-16+at+1.25.13+PM.jpeg)
KOCHA Hans Van De Pluijm yuko mbioni kujiunga
na timu ya Singinda United ambayo imepanda ligi kuu msimu ujao ikiwa ni katika
kukiboresha kikosi hicho.
Timu hiyo kwa sasa ipo chini ya mwenyekiti wa kamati ya Usajili Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye amedhamiria kufanya usajili utakaokuwa na tija.
Mwigulu ambaye ni mshabiki wa Yanga na alionesha dhahiri kutaka kuendelea kuwapo kwa Mholanzi huyo katika kikosi cha Yanga lakini ilishindikana na tayari ameshavunjiwa mkataba na wanajangwani.
Uamuzi wa Pluijm kwenda Singida ni moja ya mikakati ya Mwigulu ambaye ameweka nia ya kufanya usajili wa nguvu utakaowashangaza watu wote na sio kuletewa wachezaji watakaokuwa hawana msaada na timu.

Pluijm alikaririwa akisema kuwa atasaini
katika klabu moja wapo ya ligi kuu nchini hivi karibuni lakini sio Simba
kwahiyo hatma yake itajulikana hivi punde tu wapi atakapoelekea mholanzi huyo
na tayari ameshaonekana katika picha ya pamoja na kiungo wa kimataifa kutoka
nchini Zimbabwe aliyesajiliwa hivi karibuni.
Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo wa kimataifa Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn FC kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni usajili wa awali.
Kutinyu anayecheza ligi ya Zimbabwe atajiunga na Singida United wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi June mwaka huu.

No comments:
Post a Comment