Mamlaka zinazosimamia mashindano
mbalimbali nchini Misri zimethibitisha kuwa Rais wa Shirikisho la soka
barani Afrika CAF, Issa Hayatou atafikishwa kwa
mkurugenzi wa mashitaka kutokana na tuhuma za rushwa
zinazomkabili huku zikiwemo zile za utoaji haki za matangazo ya ligi
mbalimbali.
Mamlaka hizo
zimebainisha kuwa Hayatou alikiuka kipengele namba vifungu (A), (B),
(C), (D), (E) za sheria za uhifadhi na ulinzi wa mashindano, baada ya kukiuka
matakwa ya kazi yake na kuwapa haki za matangazo kampuni ya Lagardere Sports
pekee pasipo kuweka wazi ili kampuni nyingine zenye uwezo pia zijitokeze.
Ripoti inasema
kuwa Hayatou aliwapa Lagardere haki za matangazo kwa miaka 12 kuanzia
mwaka 2017 mpaka mwaka 2028. CAF ilisaini kandarasi na Lagardere
mwezi June 2015, ikiwa ni takribani mwaka mmoja kabla makubaliano ya haki hizo
hayajakwisha. Ni sahihi pia kusema kuwa CAF iliwapa haki
hizo Lagardere mwaka 2008 mpaka 2016, ikimaanisha kampuni hiyo
imepewa mzigo huo kwa miaka 20.
Haki hizi
hazikuwa kwa upande wa urushwaji matangazo kwa njia ya satellite peke yake bali
hata kwa wenye matumizi ya tovuti, na sio kwa Misri na Afrika peke yake,
bali dunia kwa ujumla.
Mamlaka hizo
za mashindano ya Misri, zimeomba CAF kuchukua hatua za haraka kutokana na
kifungu cha sheria namba 20 kilichopo kwenye sheria za mashindano, ikiwemo
kuvunja mkataba uliopo kati yake na Lagardere kutokana na matokeo
iliyonayo kwa Misri.
Mamlaka hiyo
pia imetoa ruksa kwa kampuni ya BeIn media pamoja na kampuni nyingine
zilizoomba haki ya kurusha matangazo mubashara kuendelea kufanya hivyo hasa kwa
ajili ya mashindano ya mataifa ya Afrika, 2017 AFCON itakayoanza January
14.
CAF iabadili
pia namna haki za matangazo za mashindano mbalimbali zinavyouzwa nchini Misri
katika mantiki ya kugawanya vifurushi vinavyohakikisha kutengeneza mazingira
yatakayovutia mahsindano hayo kurushwa na vituo.
Mamlaka za
mashindano zinaweka wazi kuwa CAF ina mlengo wa kuhakikisha inalinda na
kusimamia sheria za mashindano na pia inatakiwa kufuata hivyo kulingana
na makubaliano yaliyopo kati ya serikali ya Misri na CAF.
Na kwa
taarifa zinazoendelea kutoka ni kuwa CAF ina mpango wa kuhamisha makazi
yake kutoka nchini Misri, lakini mamlaka ya mashindano imesema kuweza
kufanya hivyo asilimia 75 ya wanachama ambao ni nchi 54 wanatakiwa kupiga kura
kukubali kwenye mkutano mkuu kutokana na sheria za CAF kifungu namba 1.
No comments:
Post a Comment