MSHAMBULIAJI Zahoro Pazi aliyesajiliwa Mbeya City amemtumia ujumbe mfupi
wa maneno (SMS) Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi
akimuomba kumsaidia ili apate ITC yake inayoshikiliwa na timu ya FC Lupopo ya
DR Congo.
Endapo Pazi atashindwa kupata ITC hiyo itakuwa vigumu kucheza mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kesho Jumamosi City wanaikaribisha Kagera Sugar na huenda akakosa mechi hiyo.
Endapo Pazi atashindwa kupata ITC hiyo itakuwa vigumu kucheza mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kesho Jumamosi City wanaikaribisha Kagera Sugar na huenda akakosa mechi hiyo.
Katika ujumbe huo, Pazi alikwenda mbali zaidi kwa kumueleza Malinzi kuwa
suala lake linafahamika huku akidai kuwa mchezo mzima ulichezwa na Mkurugenzi
wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura aliyetoa kibali chake kwenda Lupopo na sasa
TFF haimpi ushirikiano wa kupata kibali hicho.
No comments:
Post a Comment