WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape
Nnauye amefungua Tamasha la Michezo la Karatu lililofanyika leo
Mratibu wa tamasha hilo, ambaye ia ni mwanariadha
wazamani na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Meta Petro alisema, Waziri Nape ndiye alikuwa mgeni rasmi katika
tamasha hilo, ambalo hufanyika kila mwaka.
Kwa mujibu wa Petro, mchezo wa mpira wa wavu na soka,
fainali zake zilifanyika Ijumaa Desemba 16, lakini washindi watakabidhiwa
zawadi zao pamoja na wenzao wa riadha na baiskeli Jumamosi Desemba 17 siku ya
kilele cha tamasha hilo, ambalo hudhaminiwa na Olympic Solidarity kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) na FBF.
Mechi za soka na mpira wa wavu ambazo huanzia ngazi
ya chini na kushirikisha timu kibao, kabla
ya kucheza fainali na kupata washindi wa michezo hiyo, ambao hukabidhiwa zawadi
nono kutoka kwa waandaaji,
Baadhi ya zawadi zinazotolewa na Taasisi ya Filbert
Bayi Foundation (FBF), ambao ndio waandaaji ni pamoja na fedha taslimu, mipira,
nyavu za magoli ya mchezo wa soka, jezi, glovu na vifaa vingine.
Pia kwa upande wa mchezo wa mpira wa wavu, vifaa
vinavyotolewa kwa washindi mbali na fedha taslimu ni pamoja na mipira, wavu za
kuchezea na vifaa vingine vya mchezo huo, ambyo mjini Karatu huchezwa zaidi na
timu za madhehebu ya kidini.
Kwa
ujumla zawadi katika michezo mbalimbali ya Tamasha la Karatu ni za
kuvutia na zimeanufaisha wanamichezo binafsi na timu kwa kupata fedha
taslimu na vifaa vya michezo, ambavyo vinasaidia kuongeza ari ya
kushiriki katika michezo na kuinua vipaji.
No comments:
Post a Comment