WAKONGWE WALIOWAHI KUWIKA BANDARI UWANJANI KESHO
WAKALI wa kusakata
kambumbu waliowahi kuchezea timu ya Bandari ‘Bandari Veterani’ wanatarajiwa
kushuka dimbani kucheza na timu ya Bandari kesho kwenye uwanja wa Bandari
Kurasini, Dar es Salaam.
Akizungumza na gazeti hili jana, mratibu wa
mechi hiyo Kenedy Mwaisabula maarufu kama ‘Mzazi’ alisema mchezo huo wa
kufungua mwaka 2017 utaanza saa mbili asubuhi na kuwaalika wapenzi wa soka
kujionea vipaji.
“Mchezo utakuwa wa kuvutia kwani wakongwe
watakuwa na kazi ya kuwafundisha vijana namna ya kucheza soka bila kukimbizana
kwani watakuwa wanapipiga pasi moja na kuachia hivyo nawaalika wote kwani
hakuna kiingilio,” alisema Mwaisabula.
Kikosi cha Bandari cha zamani kitaundwa na
wachezaji Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Salvatory Edward, Salum Sued ‘Kusi’,
Waziri Mahadhi ‘Mandieta’, Semmy Kessy, David Beatus, Mudy Pwani, Zuberi
Katwila, Gwakisa Mwandambo.
Wengine ni Simon Butte, Juma Dallo, Jemedari Said, Husein Mataka,
Mick Zongela, Peter Nkwera, Ismail Issa, Rajab Kablao na Abdallah Rajab.
Pia
Mwaisabula alisema mchezo huo utakuwa sehemu ya kuwakutanisha wakongwe hao na
kubadilishana mawazo, kwani wengi wao inakuwa nadra kuonana baada ya kuachana
kwenye soka la ushindani na baadae watashiriki kwenye sherehe ya kukaribisha
mwaka itakayofanyika Bandari.
No comments:
Post a Comment