Pages

Friday, November 4, 2016

YANGA YAKUBALI KUILIPA SIMBA MILIONI 200 SAKATA LA HASSAN KESSY

Mazungumzo kati ya Viongozi wa Young Africans na Simba, katika shauri la madai, yanaendelea vema na mwishoni mwa wiki hii huenda wakakamilisha kwa kuridhiana.

Viongozi hao wamefanya hivyo kwa dhana kuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) inayosisitiza uungwana katika soka ikisema: “My Game is Fair Play”. Kwa upande wa Young Africans, uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit wakati upande wa Simba alikuwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.

Katika kikao hicho ambacho Msuluhishi wake, Wakili na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Said El – Maamry hakuhudhuria kwa sababu za udhuru, Baraka wa Young Africans aliongozana na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Young Africans, Omar Said pamoja na Mawakili Oscar Magolosa na Alx Mushumbusi.

Kwa hali halisi ya uchumi kwa sasa, timu hizo zimezungumza hadi kufikia mwafaka wa kiwango kisichozidi Sh milioni 200 kutoka dola dola 600,000 (zaidi ya Sh milioni 1,200 au Bilioni 1.2). Mazungumzo ya wikiendi hii yanakwenda kukamilisha mvutano wao, kama ambavyo walikubaliana kwenye kikao kilichoketi jana Novemba 03, 2016.

Madai makuu ya Simba ni dhidi ya mchezaji Hassan Hamis Ramadhani maarufu kwa jina la Hassan Kessy na dhidi ya Young kudaiwa kuvunja mkataba na kuingilia makubaliano mapya wakati tayari mchezaji alikuwa na mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment