KOCHA Mkuu mpya wa Yanga, George
Lwandamina amekanusha taarifa za kuleta
wachezaji toka Zesco lakini pia amekiri wachezaji wa Tanzania ni legelege
ukilinganisha na Zambia.
Lwandamina aliyasema hayo jana wakati
akitambulishwa rasmi kwa wandishi wa habari pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi wa
Yanga, Hans Pluigm.
Lwandamina alisema hana mpango wa
kubadilisha chochote kwenye benchi la ufundi pamoja na wachezaji huku
akikanusha kuwaleta nchini wachezaji Jesse Were na Misheck Chaila lakini akasema
amekabidhiwa jukumu zito ila analichuliwa kama changamoto kuhakikisha Yanga inafanya vema.
“Nitapambana kuhakikisha Yanga inafanya
vizuri, najua ni changamoto mpya kwangu lakini nitafanya kila linalowezekana kuhakikisha tunafanya vizuri
kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika,” alisema Lwandamina
"Nasikia
tetesi kuhusu wachezaji wapya kutoka Zesco kusajiliwa Yanga naomba ifahamike
kuwa kama kocha mkuu sijui chochote labda mchakato hiyo inafanyika bila mimi
kushirikishwa na kikosi kilichopo ndicho nitaendelea nacho" alisema
Lwandamina.
Pia Lwandamina alisema hakuna wachezaji, aliowaleta japo amekiri wachezaji wa Tanzania hawako fiziki kama wa Zambia kwani alishawaona wakati wakicheza na Ruvu Shooting kwenye mechi ya mwisho ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara

Akimzungumzia
mtangulizi wake Lwandamina amemsifu Pluijm kwa kusema amefanya kazi nzuri na
kuahidi kufuata nyayo zake kwa kushirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha
Yanga inapata mafanikio zaidi.
Nae
Mkurugenzi mpya wa ufundi Pluigm alisema yeye hana shida na kubadilishiwa
majukumu kikubwa ataendelea kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba wake.
Pluigm
alianza kuifundisha Yanga 2014 na ameiongoza katika mechi 128 kwenye awamu
mbili, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23.
Katika mechi
19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati
katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Na anahama nafasi akiwa akibeba mataji yote matatu msimu uliopita, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria.

Yanga
ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998
kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, Pluijm alishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita.
Na kwa mafanikio hayo, Pluijm alishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment